top of page

Yesu wa Uongo wa Kanisa la Kisasa

Admin
Sep 20, 2022
3 min read

Updated: 1 day ago


“Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au kama mkimpokea roho mwingine ambaye si yule mliempokea, au injili nyingine ambayo hamkuikubali, mnavumiliana naye vyema !” — Wakorintho wa pili 11:4

Yesu wa kweli ndiye yule anayelingana na maelezo ya Bibilia. Ukristo wa kweli ni ule ambao imani yake na utendaji wake unalingana na maandiko matakatifu. Walakini, kuna “Yesu mwingine” ambaye anawadanganya wakristo walio rudi nyuma au wasioongoka ilhali wanakiri kuwa wakristo. Kwa hiyo, Paulo alilazimika kufichua huyu Yesu wa uongo katika 2 wakorintho 11:4 kwa maana, kuna roho ambayo huhudumiwa na Yesu wa uongo, lakini sio Roho mtakatifu; Injili inahudumiwa na Yesu wa uongo, lakini sio Injili ya kweli ambayo huokoa nafsi.


Ni wazi kuwa si kila Yesu anayehubiriwa chini ya jua ni wa kweli. Waislamu wana Yesu wao. Wamomoni wana Yesu wao. Wakatoliki wana Yesu wao. Wayahudi wana yesu wao. Orodha inaweza kuendelea. Hata hivyo, vipi kuhusu ile aina yako unayoiita ukristo? Makanisa mengi ya kikristo yako mbali na Mungu na kinyume na maandiko matakatifu hivyo basi wanapatikana katika kundi moja. Makanisa ya kisasa wana Yesu wao! Lakini yeye sio wa kweli katika sehemu kubwa. Wakristo kwa jumla wameenda mbali sana na Mungu kwa kuwa


“JIJARIBUNI WENYEWE kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? msiwe mmekataliwa.” — Wakorintho wa pili 13:5

JIJARIBUNI WENYEWE! Je unaye Yesu wa kweli? Au ni Yesu mwingine aliyeundwa na mhubiri huko mtaani? Hii ni ibada ya sanamu! Wakati watu wanajitengenezea mungu katika akili zao anayewafaa wao wenyewe, na wanamwita mungu huyo, Yesu, huyu ndiye Yesu wa uongo wa Kanisa La Kisasa. Ni jukumu letu kutambua yesu wa kweli na yesu wa uongo. Ni jukumu letu kutambua kati ya Wakristo wa kweli na Wakristo wa uongo. Ili kufanya hivyo ni lazima tuangalie zaidi ya ule muonekano wa “ukristo” unaonyeshwa kwa nje.


“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakivaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; lakini mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” — Matayo 7:15-20

Ukristo wa karne iliyopita kwa kiasi kikubwa sio bora kuliko Uyahudi wa karne ya kwanza. Kupitia makutano mengi ya wayahudi walioongoka kwa uongo, shetani kimsingi alikuwa akimiliki Masinagogi yote ya nchi ya Israeli. Shetani alikuwa tayari na kumngojea Yesu alipokuja kwa wayahudi. Huu ulikuwa mpango wake wakati huo wote. Kwa hiyo, Yesu alipokuja kwenye uyahudi, madhehebu yote ya uyahudi yaliungana dhidi ya Masihi wao wenyewe na kumsulubisha!


Hata hivyo, hivyo ndivyo yaweza kusemwa kuhusu Ukristo Wa Kisasa. Shetani sasa anakalia majukwaa ya makanisa ya kisasa ya Mataifa! Shetani yuko tayari na anangoja kuwadanganya wakristo wa kweli, wakati na ikiwa watatia giza mlango wa kanisa la kisasa kwa kuwaingiza kwa mafundisho ya uongo. Hata hivyo, sasa, kama ilivyo katika karne ya kwanza, ni wajibu wetu kutambua na kujitambulisha na Yesu Kristo wa pekee wa Bibilia! Ni wajibu wetu kumkiri kwa uwazi Yesu wa kweli tofauti na yesu wa uwongo, na kumtangaza yule wa kweli hadharani bila haya.


“Basi, kila mtu atakaye nikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakaye nikana mbele ya watu, yeye pia nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nimekuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mama mkwe; Na Maadui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake. Apendaye baba au mama kuniliko mimi, hanistahili ; na yule apendaye mwana au binti kuniliko mimi, hanistahili. Na mtu asiyechukua msalaba wake, na kunifuata mimi, hanistahili. Mwenye kuhifadhi maisha yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza maisha yake kwa ajili yangu ataipata.” — Matayo 10:32-39
 
 
 

Comments


bottom of page