top of page

Uhusiano na Mungu

Admin
Sep 5, 2022
3 min read

Updated: 1 day ago


Je unampenda mungu?


“Ikiwa mnanipenda,hifadhi AMRI ZANGU” — Yohana 14:15

Kama unampenda Mungu, basi hifadhi AMRI zake. Huu ndio ukweli wa kibiblia!. Huwezi kusema kuwa unampenda Mungu huku hautii AMRI zake, “Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kuwa tuzi hifadhi AMRI zake; na AMRI ZAKE hazihuzunishi.” (1 Yohana 5:3) Mungu hana dhambi. Kama unampenda Mungu, basi unachukia dhambi. Usingefurahishwa nayo! Ungeichukia kabisa. Mtu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kadiri ya jinsi anavyochukia dhambi. Sahau kila tafsiri nyingine tofauti ya ukristo ambao umewahi kujifunza. Kwa maana bila utiifu wa kweli kwa mungu, kukiri kwako kuwa mkristo hakumaanishi chochote katika mwanga wa umilele.“Wanakiri kuwa wanamjua Mungu, lakini kwa matendo wanamkana, ni wenye machukizo, wasiotii, na kwa kila tendo njema wamekataliwa” (Tito 1:16).


Una uhusiano na Mungu?


Watu wengi wangejibu kwa ujasiri “Ndiyo”, kwa sababu tu wanahisi kuwa ni kweli katika mioyo yao wenyewe; au labda walikuwa na jambo fulani lililowatendekea la kiroho wakati mmoja. Hata hivyo, nabii Yeremia alionya dhidi ya haya,akisema, “Moyo ni mdanganyifu juu ya vyote, na mwovu kupindukia ; nani awezaye kuujua.” (Yeremia 17:9) Uhusiano wa kweli na Mungu hubadilisha uhusiano wako na dhambi. Njia pekee ya kuhakikisha kabisa kuwa umekuja kumjua Mungu kupitia uhusiano wa kibinafsi ni kama unazihifadhi amri za Yesu Kristo “Na katika hili twajua kuwa tunamjua yeye, ikiwa tunazishika amri zake; Yeye asemaye, ninamjua na hazishiki amri zake, ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake.” ( 1 Yohana 2:3-4) Yesu Kristo ,BWANA, hatafuti maneno mazuri, maombi ya muda mrefu na sifa za nderemo, ilhali anatafuta upendo wa kweli kutoka moyoni uletao utiifu kwa NENO.


Una uhusiano na NENO LA MUNGU?


Huwezi kuwa na uhusiano na Mungu bila kujua na kulishika NENO LAKE. Hili ni jambo la kibinafsi kwa Mungu. Yesu Kristo ndiye “NENO” (Yohana 1:1-3) Ikiwa huna uhusiano wa utukufu na Bibilia, ambayo ni NENO LA MUNGU liloandikwa, basi unaishi ukristo bila Kristo. Kulingana na Masihi hii ndio hukumu yako: “NENO langu halina nafasi ndani yako.” (Yohana 8:37). Usiruhusu hili kusemwa juu yako! “Lakini muwe watendaji wa NENO, wala msiwe wasikilizaji tu, huku mkijidanganya nyinyi wenyewe.” (Yakobo 1:22). Uhuru upatikanao ndani ya Kristo huja kupitia NENO. “Kisha Yesu akasema kwa wale Wayahudi waliomwamini, mkiendelea katika Neno langu, basi nyinyi ni wanafunzi wangu kwa kweli ; Na mtaufahamu ukweli, nao ukweli utawafanya huru.” (John 8:31-32; John 8:47)


Unapenda ulimwengu?


Watu wengi hukua na kukomaa katika Maisha kwa kujifunza njia za ulimwengu (Waefeso 2:21, 1 Yohana 4:5) Wanafanya kazi kwa bidii na kujaribu kupata mafanikio ili waishi kwa kiburi. Hivyo mwishowe wanatembea, kuzungumza, kuvaa na kutenda kama tu ulimwengu unaowazunguka ( Mithali 14:12) Hata hivyo, hii ndiyo njia pana iendayo kwenye uharibifu ambayo Yesu Kristo alizungumzia katika Mathayo 7:13-14 .Kwa kuwa ulimwengu una vita dhidi ya Mungu. Jamii ya wanadamu imeanguka (Warumi 8:6-8) Ulimwengu unaokuzunguka ni tishio kwa nafsi yako ya milele (Yohana 15:18-21) Ikiwa unafanya urafiki nayo, basi unachagua upande dhidi ya Mungu kama adui wa Mbinguni “Basi yeyote atakaye kuwa Rafiki wa dunia ni adui wa Mungu” (Yakobo 4:4) Je, unaweza kuamini hivyo? Uhusiano wa ukweli na Mungu hubadilisha uhusiano wako na ulimwengu. Wale wote walio zaliwa kwa kweli na Mungu wameuushinda ulimwengu (Yohana 5:10)!


“Usipende dunia wala vitu vilivyomo duniani. Kama mtu yeyote ataipenda dunia, upendo wa Baba haumo ndani yake. Maana vyote vilivyomo duniani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi ya maisha,sio vya Baba bali ni vya dunia.Nayo dunia inapita na tamaa zilizomo:lakini yule afanyaye mapenzi ya Mungu huishi milele.” — 1 John 2:15-17.
 
 
 

Comments


bottom of page